Hatimae meneja Rafael Benitez ataondoka Chelsea akiwa na tabasabu baada ya timu yake kubeba ubingwa wa Kombe la Europa League kwa kuifunga timu ya Benfica ya Ureno 2-1 usiku wa Jumatano katika uwanja wa Amsterdam, Uholanzi.
Hii ni baada ya Branislav Ivanovic
kufunga bao maridadi kwa kichwa wakati wa muda wa ziada wa majeruhi.
Tangu alipoingia Chelsea kama kaimu
mkufunzi Benitez amekuwa na wakati mgumu kwani mashabiki wa Old Trafford
wamekuwa hawampendi.
Lakini baada ya kuifunga Benfica
mashabiki hao hao ambao walikuwa hawampendi Benitez waliishangilia ushindi wa
timu yao kwa vifijo na nderemo huku wakisahau chuki waliokuwa nao kwa kaimu
meneja huyo.
Mwaka jana Chelesea ilishinda Kombe
la Klabu bingwa bara Ulaya na mwaka huu wamebeba kombe la Europa League.
Bao lakwanza la Chelsea lilifungwa
na mshambulizi Fernando Torres nao Benfica wakapata lao kupitia mwaju wa
penalti uliofungwa na Oscar Cardozo.
Ushindi wa Chelsea unamfanya Rafael
Benitez kuwa meneja wa nne kushinda kombe la Klabu Bingwa Uropa na la Europa
League zaidi ya mara mmoja.
Wengine amabo wamewahi kushinda
kumbe hilo zaidi ya mara moja ni Giovanni Trapattoni: 1977 (Juventus); 1991
(Inter); 1993 (Juventus) ,Luis Molowny: 1985 & 1986 (Real Madrid) Juande
Ramos: 2006 & 2007 (Sevilla).