Frank Lampard amesema anaamini kuwa Jose Mourinho anaweza kuandikisha matokeo mema kwa mara nyingine kama alivyofanya wakati alipoteuliwa kocha wa Chelsea kwa mara ya kwanza ikiwa atarejea tena.
Ripoti zinasema kuwa
kocha huyo mwenye umri wa miaka 50, anakaribia kuihama klabu ya Read Madrid,
kuchukua mahala ka kaimu kocha wa klabu hiyo kwa sasa Rafael Benitez.
Lampard, ambaye
alisaini mkataba wa mwaka mmoja zaidi la Chelsea siku ya Alhamisi, ameiambia
BBC kuwa, haiwezekani kwa kocha huyo kurejea na kutulia na kutegemea rekodi
yake ya zamani.
Amesema, ikiwa
atarejea kwa mara nyingine, Chelsea huedna ikaibuka na ushindi mkubwa msimu
ujao.
Akiwa Chelsea, Morinho
alishinda vikombe sita katika kipindi cha miaka mitatu, viwili vikiwa vya ligi
kuu ya premier, lakini alijiuzulu Septemba mwaka wa 2007, baada ya uhusiano
wake na mmiliki wa klabu hiyo Roman Ambramovich kusambaratika.
Morinho alijiunga na
klaby ya Inter Millan Juni mwaka wa 2008, ambako alishinda vikombe zaidi, moja
la Bara Ulaya na vingine viwili vya ligi kuu ya Serie a.
Mwaka wa 2010,
alijiunga na Klabu ya Real Madrid na mwaka wake wa kwanza alishinda kombe la
Copa del Rey kabla ya kunyakuwa ubingwa wa ligi kuu ya La Liga kutoka kwa
vigogo wa soka nchini Uhispania Barcelona.
Kurejea kwa Mourinho,
kunakisiwa kuwa sababu kubwa ya Kandarasi ya Frank Lampard kuongezwa kwa mwaka
mmoja zaidi.
Wiki iliyopita Lampard
aliandikisha historia ya kuwa mchezaji wa Chelsea aliyefunga idadi kubwa zaidi
ya magoli, baada ya kuvunja rekodi iliyowekwa na Tambling ya magoli 202.
Lampard amefunga
magoli 203.
BBC.